KANUNI YA KUVUNA CHOCHOTE

KANUNI YA KUVUNA CHOCHOTE
 • MAVUNO NI MOJA YA MATARAJIO YA MTU BINAFSI,KANISA,TAIFA NA MBIGU.
 • VITU VITATU(3) ILI UVUNE:-
 1. LAZIMA UWE NA SHAMBA
 2. LAZIMA UWE NA MBEGU
 3. LAZIMA UZINGATIE MAJIRA.
 • MBEGU-ni chochote mtu alichonacho kwa wakati huo inaweza ikawa elimu,fedha,cheo,watoto,computer,ufundi,ubunifu,n.k
 • AINA ZA MBEGU
 1. sadaka ya upendo
 2. sadaka ya zaka au fungu la kumi(10%)
 3. sadaka ya malimbuko
 4. sadaka ya shukurani
 5. sadaka ya nadhiri
 6. sadaka ya mapatano au changizo
 • MAJIRA-ni uhitaji uliopo kwa wakati husika.
 • SHAMBA-ni kazi ya MUNGU.

THE HOLY SONG

JAMANI MUNGU YUPO (MY BROTHER AND MY SISTER GOD WELCOME TO SHARE THE SONGS AND GOOD NEWS OF JESUS CHRIST)

KUKATALIWA KWA YESU HUKO NAZARETI

KUKATALIWA KWA YESU HUKO NAZARETI
 • KWELI KUU;kama wakristo wanaomfuata Kristo,sisi tunatakiwa kuwa tayari kukabiliana na kutokueleweka na kupingwa.
 • MSTARI WA KUKUMBUKA;"Yesu akawaambia,Nabii hakosi heshima,isipokuwa katika nchi yake mwenyewe na kwa jamaa zake,na nyumbani kwake".marko 6:4
 • MAANDIKO YA SOMO:LUKA 4:16-30.
 • UTANGULIZI
 1. YESU kabla ya huduma yake alibatizwa kwanza na YOHANA mbatizaji akiwa na miaka 30.
 2. alipomaliza kubatizwa akajaa ROHO MTAKATIFU akamwongoza nyikani(akafunga siku 40)
 3. kumbuka kwamba nyumbani kwake YESU kulikuwa Galilaya.
 4. Yesu alitenda muujiza wake wa kwanza huko KANA.
 5. YESU alikuwa na upako usio wa kawaida wa kutenda miujiza na uponyaji na kutoa unabii.
 6. YESU alikuwa ni watofauti na wengine humo mjini kwao Nazareti
 7. watu wengi wamezoea kufanya vitu virahisi tu bali vile vigumu wanaviepuka.
 8. YESU ndiye alisema nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe alitoa mfano wa nabii Eliya na Elisha walivyokataliwa na watu wa nchi yao.
 • HITIMISHO
 1. YESU alitaka kuwawa kwa kutupwa kutoka juu ya mlima lakini YESU aliweza kupita katikati ya watu hao na kuepuka kifo.

MAOMBI YA MUDA MREFU

MAOMBI YA MUDA MREFU
"MATHAYO 26:36-42.KISHA YESU AKAENDA PAMOJA NAO MPAKA BUSTANI IITWAYO GETHSEMANE,AKAWAAMBIA WANAFUNZI WAKE,KETINI HAPA,HATA NIENDE KULE NIKAOMBE.AKAMCHUKUA PETRO NA WALE WANA WAWILI WA ZEBEDAYO AKAANZA KUHUDHUNIKA NA KUSONONEKA.NDIPO AKAWAAMBIA,ROHO YANGU INA HUZUNI NYINGI KIASI CHA KUFA;KAENI HAPA,MKESHE PAMOJA NAMI.AKAENDELEA MBELE KIDOGO AKAANGUKA KIFULIFULI,AKAOMBA,AKISEMA,BABA YANGU,IKIWEZEKANA,KIKOMBE HIKI KINIEPUKE;WALAKINI SI KAMA NITAKAVYO MIMI,BALI KAMA UTAKAVYO WEWE.AKAWAJIA WALE WANAFUNZI ,AKAWAKUTA WAMELALA,AKAMWAMBIA PETRO,JE! HAMKUWEZA KUKESHA PAMOJA NAMI HATA SAA MOJA! .KESHENI,MWOMBE,MSIJE MKAINGIA MAJARIBUNI;ROHO I RADHI,LAKINI MWILI NI DHAIFU.AKAENDA TENA MARA YA PILI,AKAOMBA AKISEMA,BABA YANGU,IKIWA HAIWEZEKANI KIKOMBE HIKI KINIEPUKE NISIPOKUNYWA,MAPENZI YAKO YATIMIZWE."

 • YESU alipokuwa katika bustani ya gethsemane ndipo alipo gundua kazi iliyo baki ni kubwa sana aliyo tumwa kufanya ,ndipo aliamua kujitenga kidogo na wakina petro akiomba kuongezewa Muda na BABA YAKE kama ikiwezekana lakini muda aliopewa ulikuwa umekwisha.
 •  Ndipo YESU akahuzunika sana na kujihisi kufa na hata akaomba usiku kucha labda ataongezewa muda wa kufanya kazi ya BABA YAKE lakini haikuwezekana kwa sababu MUNGU huwa ni mtu wa muda hachelewi wala hakawii.
 • Hivyo ilimbidi YESU aombe hadi jasho lililo mtoka ni damu kabisa likadondoka mahali alipokuwa ameinamisha uso wake.
 • Hivyo tunajifunza kuwa hata kama umepakwa mafuta na MUNGU ,wewe ni mwinjilisti,nabii,mtume,mchungaji  au mwalimu  ujue unafanya hiyo kazi kwa muda MUNGU alio upanga mwenyewe hivyo fanya kwa bidii sana maana utatamani uongezewe muda haitawezekana wanatakiwa waingie watu wengine au chombo kipya cha MUNGU
 • FAIDA YA MAOMBI YA MUDA MREFU
 1. Unapata nguvu nyingi za kupambana na milango ya giza na kuwa mshindi.
 2. Unapata nguvu ya kushinda majaribu
 3. Unapata mazingira ya kukaa katika utukufu wa MUNGU.
 4. Unapata amani ya kufanya maamuzi sahihi.
 5. Unapata nafasi kubwa sana ya kusikiizwa na MUNGU.

MLANGO WA SITA (SIXTH SENSE)

MLANGO WA SITA (SIXTH SENSE)
 • MLANGO WA SITA NI MLANGO WA UFAHAMU WA MWANADAMU ULIO NA HADHINA YA VITU VITUKUFU KWA DUNIA NA MBINGUNI.
 • BINADAMU WA KAWAIDA ANA MILANGO TANO(5) AMBAYO;- 
 1. MACHO- KUONA
 2. MASIKIO-KUSIKIA
 3. ULIMI- KUONJA
 4. PUA -KUNUSA
 5. NGOZI -KUHISI
 • MLAMGO WA SITA NI MLANGO WA ROHOMTAKATIFU
 • BAADA YA ANGUKO LA ADAMU NA HAWA KATIKA BUSTANI YA EDENI HUU MLANGO ULUFUNGWA KABISA.
 • BAABA YA UUJIU YA YESU CHRISTO ALIKWENDA KUCHUKUWA FUNGUO ZILIPOKUWA ZIMEFICHWA NA KUUWEKA WAZI MLANGO HUU KWA YEYOTE ANAYETAKA KUINGIA AINGIE ALE ,ANYWE,NA ASIWE NA NJAA AU KIWI KAMWE.
 • MLANGO WA SITA NI MLANGO ALIOPEWA MTUME PETRO KWAMBA CHOCHOTE ATAKACHO FUNGA DUNIANI KITAFUNGWA NA MBINGUNI NA CHOCHOTE ATAKACHOFUNGUA DUNIANI KITAFUNGULIWA NA MBINGUNI.
 • MLANGO WA SITA NI MLANGO UNAOLETA MIUJIZA YA AJABU KUTOKA MBINGUNI NA NI MLANGO WA PEKEE AMBAO BIBLIA INASEMA NJIA ILE NI NYEMBAMBA NA WAENDAO HUKU NI WACHACHE.
 • NDUGU YANGU MTUME PETRO ALITUMIA MLANGO HUU HADI DUNIA IKASHANGAA PETRO MTU AMBAYE SIO ENGINEER,SIO PROFESSOR,WALA SIO DAKITALI INAKUWAJE WATU WANAPONYWA KWA HUU MLANGO WA SITA.
 • NDUGU YANGU PETRO ALIKUWA NI MTU WA KAWAIDA LAKINI AILETA UAMSHO MKUBWA SANA KATIKA KUUTUMIA MLANGO HUU WA SITA.
JINSI YA KUUPATA MLANGO WA SITA
 • TUBU NA UBATIZWE NA MAJI NA MOTO WA ROHO MTAKATIFU
 • POKEA KARAMA ZA ROHOMTAKATIFU
 • OMBA KILA SIKU KWA KUNENA KWA LUGHA-KUNENA KWA LUGHA NI HALI YA JUU YA KUOMBA HADI MLANGO HUO UNAFUNGUKA
 • PENDA KUOMBA BINAFSI HASA ASUBUHI NA USIKU WA MANANE
 •  PENDA KUSOMA BIBLIA 
 1. FAIDA ZA KUWA NA MLANGO WA SITA
 • MUNGU ANAKUTUMIA SANA-MAENEO YOTE
 • MUNGU ANATUKUZWA KUPITIA WEWE
 • UNAKUWA WAKILI SAHIHI WA MUNGU-KWA KUWA UNA VIPAWA VYA ROHOMTAKATIFU
 • UTUKUFU WA MUNGU UNAKUFUNIKA
 • UNAKUWA MBARIKIWA
 1. MWISHO
 • MLANGO WA SITA NI AKILI ISIYOKUWA NA UKOMO.

WAKILI WA KRISTO

WAKILI WA KRISTO
1WAKORINTHO 4:1-2
MAANA YA WAKILI
WAKILI -NI MTU ANAYE SIMAMIA MALI YA MTU MWINGINE
 1. MTUMISHI WA KRISTO NA MSIMAMIZI WA SIRI ZA MUNGU
 2. MKRISTO YOYOTE NI WAKILI WA MUNGU
 •  KANUNI ZA UWAKILI WA KRISTO
 1. ANATAKIWA KUFANYA MAPENZI YA MUNGU -1WAKOR 6:19-20
 2. ANATAKIWA ATOE HESABU YA UWAKILI MBELE ZA MUNGU -MATHAYO25:14-30

 • WAJIBU WA WAKILI
 1. KUJITOA KUTUMIKA KAMA WAKILI MWEMA-2WAKOR 8:1-8
 2. KUUKOMBOA WAKATI -LUKA 12:45-48

YESU MCHUNGAJI MWEMA

 YESU MCHUNGAJI MWEMA
Zaburi 23:1-6
"BWANA ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.katika malisho ya majani mabichi hunilaza kando ya maji ya utulivu huniongoza .Hunihuisha nafsi yangu na kuniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.Naam nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,sitaogopa mabaya;kwa maana wewe upo pamoja nami,Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.Waandaa meza mbele yangu machoni pa watesi wangu.Umenipaka mafuta kichwani pangu,Na kikombe changu kinafurika.Hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu;Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele

MCHUNGAJI MWEMA-ANAWAPA CHAKULA KONDOO WAKE MARISHO KWA WAKATI UNAOFAA
FAIDA YA KUBALI MARISHO YA MUNGU
 • TUNAPATA UTOSHEREVU WA MAISHA YA ROHONI NA MWILINI
 • TUNAPATA MIUJIZA YA KIROHO ISIYO YA KAWAIDA
 • TUNAPATA MAONGOZI YA ROHO MTAKATIFU
 • ANATUPA MAHITAJI YETU YOTE
 1. MCHUNGAJI NDIYE ANAYE JUA MAJIRA YA CHAKULA CHA MIFUGO YAKE
 2. SI KAZI YA KUNDI KUJUA LITAKULA NINI KWA WAKATI GANI BALI NI KAZI YA MCHUNGAJI MWEMA
 3. KONDOO ANAPASWA AONGOZWE NA MCHUNGAJI
 4. KONDOO ANAPASWA AKUBALI KUKAA KWENYE KUNDI ILIAPATE CHAKULA
 5. KONDOO KUKUBALI KUKAA KWENYE KUNDI NA CHINI YA MUNGU UTAFUNGULIWA HADHINA YA MBINGUNI NA KULA PAMOJA NA MUNGU
 • MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUNDI
 1. UNAPASWA UWE MNYENYEKEVU
 2. UNAPASWA UWE MTII NA MSIKIVU WA SAUTI YA MCHUNGAJI WAKO
 3. UNAPASWA KUWA NA USHIRIKIANO NA KONDOO WENZAKO
 4. UNAPASWA UJUE NA UTAMBUE MAHITAJI YAKO KWA WAKATI ILI UTIMIZIWE KIU YAKO