Showing posts with label MAOMBI YA MUDA MREFU. Show all posts
Showing posts with label MAOMBI YA MUDA MREFU. Show all posts

MAOMBI YA MUDA MREFU

MAOMBI YA MUDA MREFU
"MATHAYO 26:36-42.KISHA YESU AKAENDA PAMOJA NAO MPAKA BUSTANI IITWAYO GETHSEMANE,AKAWAAMBIA WANAFUNZI WAKE,KETINI HAPA,HATA NIENDE KULE NIKAOMBE.AKAMCHUKUA PETRO NA WALE WANA WAWILI WA ZEBEDAYO AKAANZA KUHUDHUNIKA NA KUSONONEKA.NDIPO AKAWAAMBIA,ROHO YANGU INA HUZUNI NYINGI KIASI CHA KUFA;KAENI HAPA,MKESHE PAMOJA NAMI.AKAENDELEA MBELE KIDOGO AKAANGUKA KIFULIFULI,AKAOMBA,AKISEMA,BABA YANGU,IKIWEZEKANA,KIKOMBE HIKI KINIEPUKE;WALAKINI SI KAMA NITAKAVYO MIMI,BALI KAMA UTAKAVYO WEWE.AKAWAJIA WALE WANAFUNZI ,AKAWAKUTA WAMELALA,AKAMWAMBIA PETRO,JE! HAMKUWEZA KUKESHA PAMOJA NAMI HATA SAA MOJA! .KESHENI,MWOMBE,MSIJE MKAINGIA MAJARIBUNI;ROHO I RADHI,LAKINI MWILI NI DHAIFU.AKAENDA TENA MARA YA PILI,AKAOMBA AKISEMA,BABA YANGU,IKIWA HAIWEZEKANI KIKOMBE HIKI KINIEPUKE NISIPOKUNYWA,MAPENZI YAKO YATIMIZWE."

  • YESU alipokuwa katika bustani ya gethsemane ndipo alipo gundua kazi iliyo baki ni kubwa sana aliyo tumwa kufanya ,ndipo aliamua kujitenga kidogo na wakina petro akiomba kuongezewa Muda na BABA YAKE kama ikiwezekana lakini muda aliopewa ulikuwa umekwisha.
  •  Ndipo YESU akahuzunika sana na kujihisi kufa na hata akaomba usiku kucha labda ataongezewa muda wa kufanya kazi ya BABA YAKE lakini haikuwezekana kwa sababu MUNGU huwa ni mtu wa muda hachelewi wala hakawii.
  • Hivyo ilimbidi YESU aombe hadi jasho lililo mtoka ni damu kabisa likadondoka mahali alipokuwa ameinamisha uso wake.
  • Hivyo tunajifunza kuwa hata kama umepakwa mafuta na MUNGU ,wewe ni mwinjilisti,nabii,mtume,mchungaji  au mwalimu  ujue unafanya hiyo kazi kwa muda MUNGU alio upanga mwenyewe hivyo fanya kwa bidii sana maana utatamani uongezewe muda haitawezekana wanatakiwa waingie watu wengine au chombo kipya cha MUNGU
  • FAIDA YA MAOMBI YA MUDA MREFU
  1. Unapata nguvu nyingi za kupambana na milango ya giza na kuwa mshindi.
  2. Unapata nguvu ya kushinda majaribu
  3. Unapata mazingira ya kukaa katika utukufu wa MUNGU.
  4. Unapata amani ya kufanya maamuzi sahihi.
  5. Unapata nafasi kubwa sana ya kusikiizwa na MUNGU.