KUKATALIWA KWA YESU HUKO NAZARETI

KUKATALIWA KWA YESU HUKO NAZARETI
 • KWELI KUU;kama wakristo wanaomfuata Kristo,sisi tunatakiwa kuwa tayari kukabiliana na kutokueleweka na kupingwa.
 • MSTARI WA KUKUMBUKA;"Yesu akawaambia,Nabii hakosi heshima,isipokuwa katika nchi yake mwenyewe na kwa jamaa zake,na nyumbani kwake".marko 6:4
 • MAANDIKO YA SOMO:LUKA 4:16-30.
 • UTANGULIZI
 1. YESU kabla ya huduma yake alibatizwa kwanza na YOHANA mbatizaji akiwa na miaka 30.
 2. alipomaliza kubatizwa akajaa ROHO MTAKATIFU akamwongoza nyikani(akafunga siku 40)
 3. kumbuka kwamba nyumbani kwake YESU kulikuwa Galilaya.
 4. Yesu alitenda muujiza wake wa kwanza huko KANA.
 5. YESU alikuwa na upako usio wa kawaida wa kutenda miujiza na uponyaji na kutoa unabii.
 6. YESU alikuwa ni watofauti na wengine humo mjini kwao Nazareti
 7. watu wengi wamezoea kufanya vitu virahisi tu bali vile vigumu wanaviepuka.
 8. YESU ndiye alisema nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe alitoa mfano wa nabii Eliya na Elisha walivyokataliwa na watu wa nchi yao.
 • HITIMISHO
 1. YESU alitaka kuwawa kwa kutupwa kutoka juu ya mlima lakini YESU aliweza kupita katikati ya watu hao na kuepuka kifo.